Mbeya City imeanza vizuri mchezo wake wa NBC Premier League baada ya kuichapa Singida Black Stars kwa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Riphati Msuya dakika ya 22, likitosha kuipa Mbeya City ushindi mbele ya mashabiki wake.
Matokeo hayo yanaifanya Singida Black Stars kuondoka mikono mitupu katika safari yake ya ugenini, huku Mbeya City ikivuna pointi tatu muhimu katika kampeni zake za ligi.
ADVERTISE HERE