Timu ya taifa ya England imemtangaza kiungo Jobe Bellingham katika kikosi chake kwa mara ya kwanza, hatua inayofungua uwezekano wa kuwaona ndugu hao wawili, Jobe na Jude Bellingham, wakicheza pamoja katika timu ya taifa.
Wakati Jobe akipata nafasi hiyo kwa mara ya kwanza, kiungo mshambuliaji Cole Palmer ameachwa nje ya kikosi kilichotangazwa.
Kikosi hicho kimejumuisha makipa Pickford, Steele na Trafford. Katika safu ya ulinzi wamo Branthwaite, Guéhi, Hall, Konsa, Quansah, Spence, Trent na White.
Viungo walioitwa ni Anderson, Jude Bellingham, Eze, Garner, Jobe Bellingham, King, Lewis-Skelly na Rice, huku safu ya ushambuliaji ikiwa na Calvert-Lewin, Gibbs-White, Gordon, Kane, Ngumoha na Rogers.
ADVERTISE HERE