Barcelona imepata ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya Atletico Madrid katika mchezo wa La Liga uliopigwa kwenye dimba la Metropolitano, matokeo yanayoifanya timu hiyo kuongeza uongozi wake kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi tatu.
Atletico Madrid ndiyo ilianza kupata bao kupitia Giuliano Simeone dakika ya 10, kabla ya kiungo Fermin Lopez kuisawazishia Barcelona dakika ya 45. Fermin alirudia tena dakika ya 66 akimalizia pasi ya Lamine Yamal na kuipa Barcelona ushindi wa mabao 2-1.
Ushindi huo unaendeleza msimu mzuri wa Fermin Lopez, ambaye hadi sasa amehusika moja kwa moja katika mabao 15 ya Barcelona ndani ya michezo 15 aliyocheza, akifunga mabao nane na kutoa pasi saba za mabao.
Kwa upande mwingine, Lamine Yamal amefikisha jumla ya mchango wa mabao 30 msimu huu, akihusisha mabao aliyofunga na pasi za mwisho alizotoa, licha ya msimu kuwa bado katika hatua za mwanzo.
Ni ushindi mkubwa kwa kikosi cha Hansi Flick, ambacho kimeendelea kuimarisha nafasi yake katika mbio za ubingwa wa La Liga.