Sundowns wamnyemelea Barker, Simba kumlinda kwa gharama yoyote

Joel JJ By Joel JJ
‱
11m ago
Sundowns wamnyemelea Barker, Simba kumlinda kwa gharama yoyote

Uongozi wa Simba SC umeweka msimamo wake kuhusu mustakabali wa Kocha Mkuu Steve Barker, kufuatia taarifa zinazomuhusisha na klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, huku mabosi wa Msimbazi wakipanga kumuongezea mkataba mpya wa muda mrefu.

Licha ya tetesi zinazozidi kusambaa kuhusu nia ya Sundowns kumtaka kocha huyo, taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa klabu hiyo haina mpango wa kumuachia Barker kwa sasa.

Badala yake, viongozi wa Simba wameanza mikakati ya kuhakikisha kocha huyo anaendelea kusalia Msimbazi kwa muda mrefu zaidi, ikiwa ni pamoja na kumpatia mkataba mpya wenye maslahi bora.

Hivi karibuni, Mamelodi Sundowns ilihusishwa na mpango wa kumchukua Barker ili akachukue nafasi ya Miguel Cardoso, jambo lililoibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wa Simba wanaotaka kocha huyo aendelee na kazi yake.

Tangu alipokabidhiwa mikoba ya kuinoa Simba mwezi Desemba 2025, Barker amekuwa sehemu muhimu ya mipango ya kurejesha ushindani ndani ya kikosi hicho, hali iliyoongeza imani ya uongozi na mashabiki kwake.

Chanzo cha ndani ya klabu hiyo kimeeleza kuwa Barker ana furaha ya kuendelea kufanya kazi Tanzania na kwamba mazungumzo ya kumuongezea mkataba tayari yapo kwenye mipango ya viongozi.

"Barker bado yupo sana Msimbazi na anafurahia maisha ya hapa. Sundowns wanaweza kuwa wanamtaka kwa sababu ni kocha mkubwa, lakini ukweli ni kwamba hakuna uwezekano wa yeye kuondoka. Uongozi tayari upo kwenye mazungumzo ya kumuongezea mkataba mpya na mnono wa muda mrefu ili kulinda benchi letu la ufundi," kilieleza chanzo hicho.

Mkataba wa sasa wa Barker unatarajiwa kumalizika mwanzoni mwa mwaka 2027, hivyo Simba imeona umuhimu wa kuanza mapema mazungumzo ya kuongeza muda wa ushirikiano wao ili kuepusha sintofahamu kuhusu mustakabali wa benchi la ufundi.

Kwa upande wa malengo ya klabu, Simba inataka kuendeleza ubora wake katika mashindano ya ndani huku ikiweka nguvu zaidi katika kampeni za Ligi ya Mabingwa Afrika.

ADVERTISE HERE

More Stories

Singida BS yafafanua sababu ya kuwaacha baadhi ya mastaa
Singida BS yafafanua sababu ya kuwaacha baadhi ya mastaa
19m ago
READ MORE →
Rasmi: Caf yaidhinisha uwanja wa Uhuru kwa mechi za Simba na Yanga
Rasmi: Caf yaidhinisha uwanja wa Uhuru kwa mechi za Simba na Yanga
23m ago
READ MORE →
Hatma ya Carrick na Man united iko hatiani, Pochettino na Eddie Howe wakitajwa
Hatma ya Carrick na Man united iko hatiani, Pochettino na Eddie Howe wakitajwa
1h ago
READ MORE →
Wenger autaka Urais wa Fifa, Kupambana na Infantino
Wenger autaka Urais wa Fifa, Kupambana na Infantino
3h ago
READ MORE →
Kikosi bora cha mwaka 2026 chatajwa, Messi na Mbappé waongoza safu ya ushambuliaji
Kikosi bora cha mwaka 2026 chatajwa, Messi na Mbappé waongoza safu ya ushambuliaji
13h ago
READ MORE →
Mbappé atwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba La Liga
Mbappé atwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba La Liga
13h ago
READ MORE →
Pau CubarsĂ­ atwaa tuzo ya Golden Boy 2026
Pau CubarsĂ­ atwaa tuzo ya Golden Boy 2026
17h ago
READ MORE →
Thomas Frank aingia kwenye rada za Crystal Palace huku presha ikimkabili Pierre Sage
Thomas Frank aingia kwenye rada za Crystal Palace huku presha ikimkabili Pierre Sage
1d ago
READ MORE →
Penalti ya Sunderland dhidi ya Chelsea yazua mjadala, VAR yaibua maswali
Penalti ya Sunderland dhidi ya Chelsea yazua mjadala, VAR yaibua maswali
1d ago
READ MORE →
Nado aongezwa kikosi cha Taifa Stars kinachokwenda kuikabili Nigeria
Nado aongezwa kikosi cha Taifa Stars kinachokwenda kuikabili Nigeria
1d ago
READ MORE →