Crystal Palace yamfuta Pierre Sage baada ya mechi 16, Thomas Frank atajwa kumrithi

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
12 Nov 2026
Crystal Palace yamfuta Pierre Sage baada ya mechi 16, Thomas Frank atajwa kumrithi

Klabu ya Crystal Palace imethibitisha kumfuta kazi kocha wake mkuu, Pierre Sage, baada ya kuiongoza timu hiyo katika michezo 16 pekee. Uamuzi huo umefanyika Jumatatu, huku matokeo ya timu hiyo yakiwa sababu ya mabadiliko hayo.

Katika michezo hiyo 16, Sage alifanikiwa kupata ushindi mara tano, sare tatu na kupoteza michezo minane, rekodi iliyomuweka kwenye presha ya kuendelea kuinoa timu hiyo.

Kuondoka kwa Sage kunafanya kuwa mara ya sita katika historia ya Ligi Kuu England kwa makocha wawili kuondoka kwenye nafasi zao siku moja ndani ya msimu mmoja. Tukio hilo linahusisha pia Michael Carrick, aliyeondoka kwenye nafasi yake siku hiyo hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa, Sage anatarajia kuchukua mapumziko baada ya kuondoka Crystal Palace, huku kukiwa hakuna mazungumzo yaliyofikia hatua ya juu kati yake na klabu ya RC Lens.

Kwa upande wa wanaoweza kumrithi, kocha Thomas Frank anatajwa kuwa kinara kwenye orodha ya wagombea wa nafasi hiyo.

More Stories

Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
5h ago
READ MORE β†’
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
11h ago
READ MORE β†’
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
11h ago
READ MORE β†’
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
14h ago
READ MORE β†’
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
14h ago
READ MORE β†’
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
15h ago
READ MORE β†’
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
16h ago
READ MORE β†’
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
17h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
19h ago
READ MORE β†’