Uruguay yaichapa Argentina 2-1 katika mchezo wa kwanza baada ya Messi kuondoka

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
14 Nov 2026
Uruguay yaichapa Argentina 2-1 katika mchezo wa kwanza baada ya Messi kuondoka

Timu ya taifa ya Argentina imeanza vibaya kipindi kipya kinachofuata baada ya Lionel Messi, ikikubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Uruguay katika mchezo uliopigwa dimba la Bombonera. Mchezo huo pia umekuja wakati kocha Lionel Scaloni akiongeza mkataba wake hadi mwaka 2030.

Uruguay ilionyesha uwezo wa kudhibiti mchezo, ingawa haikuwa na ubunifu mkubwa katika mashambulizi. Argentina nayo ilipata nafasi kadhaa kupitia Julian Alvarez na Enzo Fernandez, lakini kipa wa Uruguay alifanya kazi nzuri kuzuia jitihada zao.

Licha ya Uruguay kutofanya shambulizi lolote lililoelekezwa langoni katika kipindi cha kwanza, ilifanikiwa kupata bao la kuongoza kupitia mpira wa adhabu. Mpira uliotolewa na Lisandro Martinez ulimpiga Balerdi usoni na kuelekea moja kwa moja wavuni, na kuifanya Uruguay kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili Uruguay iliongeza bao la pili kupitia kona, ambapo Ronald Araujo aligusa mpira kwa kichwa na kuuelekeza wavuni kwa namna isiyotarajiwa. Hata hivyo, Argentina ilijaribu kurejea mchezoni baada ya kuingia kwa Prestianni, ambaye aliongeza kasi na kuanzisha mashambulizi kadhaa.

Dakika ya 72, Prestianni alimpa pasi Julian Alvarez aliyemalizia kwa ustadi na kuifungia Argentina bao la kufutia machozi. Argentina ilijaribu kusaka bao la kusawazisha, lakini Uruguay iliimarisha ulinzi na kulinda ushindi huo muhimu wa mabao 2-1.

More Stories

Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
5h ago
READ MORE β†’
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
11h ago
READ MORE β†’
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
11h ago
READ MORE β†’
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
14h ago
READ MORE β†’
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
14h ago
READ MORE β†’
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
15h ago
READ MORE β†’
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
16h ago
READ MORE β†’
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
17h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
19h ago
READ MORE β†’