Mataifa tisa yafuzu Afcon 2027: Senegal, Mali, Morocco kuungana na wenyeji

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
2d ago
Mataifa tisa yafuzu Afcon 2027: Senegal, Mali, Morocco kuungana na wenyeji

Mataifa tisa tayari yamejihakikishia nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 zitakazopewa jina la PAMOJA, baada ya kukamilika kwa mechi za raundi ya nne ya kufuzu zilizochezwa Novemba 16 na 17, 2026.

Mataifa hayo ni wenyeji wenza Tanzania, Kenya na Uganda, pamoja na Morocco, Burkina Faso, Benin, Mali, Cameroon na Senegal ambazo zimepata tiketi kupitia matokeo ya mechi za kufuzu. Morocco, bingwa mtetezi, imekuwa miongoni mwa timu zilizofuzu baada ya kuifunga Niger bao 1-0 na kufikisha pointi 12 katika Kundi A.

Kwa mujibu wa CAF, timu hizo sita zimeungana na wenyeji watatu na kufanya idadi ya washiriki waliothibitisha kufuzu kufikia tisa kati ya 24 watakaoshiriki fainali hizo. Hii ina maana kuwa nafasi nyingine 15 bado zitasubiriwa katika mechi mbili za mwisho za kufuzu zitakazochezwa Machi 2027.

Fainali za AFCON 2027 zinatarajiwa kufanyika kuanzia Juni 19 hadi Julai 17, 2027, katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Michuano hiyo itakuwa ya kihistoria kwa Afrika Mashariki, kwani kwa mara ya kwanza nchi tatu zitakuwa mwenyeji wa pamoja wa fainali za AFCON.

More Stories

Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
5h ago
READ MORE β†’
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
11h ago
READ MORE β†’
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
11h ago
READ MORE β†’
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
14h ago
READ MORE β†’
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
14h ago
READ MORE β†’
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
15h ago
READ MORE β†’
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
16h ago
READ MORE β†’
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
17h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
19h ago
READ MORE β†’