Yanga katika mtihani wa Polisi Tanzania

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1d ago
Yanga katika mtihani wa Polisi Tanzania

Kikosi cha Yanga kimejipanga kusaka pointi tatu ugenini kitakaposhuka dimbani kesho Ijumaa, Novemba 20, 2026, kuikabili Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa kwenye Uwanja wa Ushirika, Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Wananchi hao wanarejea katika mikikimikiki ya ligi kuu baada ya mapumziko ya kupisha michezo ya kimataifa ya timu za taifa (FIFA Break), huku wakiwa wametumia sehemu ya mapumziko hayo kufanya maandalizi kupitia kambi yao ya Zanzibar.

Kocha wa mipira ya kutenga wa Yanga, Kagisho Dikgacoi, amesema maandalizi ya kikosi hicho yamekwenda vizuri, huku akionyesha kuridhishwa na namna wachezaji wanavyopokea mbinu za kocha mpya.

β€œTunaamini timu ipo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Polisi Tanzania. Tulifanya maandalizi mazuri kupitia kambi yetu ya Zanzibar, ambapo wachezaji wameonesha mwitikio mzuri kwa kocha mpya na mbinu mpya za kiufundi tunazoanza kuzifanyia kazi,” amesema Dikgacoi.

Matumaini ya Yanga kufanya vizuri katika mchezo huo yameongezeka baada ya wachezaji waliokuwa kwenye majukumu ya timu zao za taifa kurejea kikosini na kuungana na wenzao.

Dikgacoi amesema wachezaji wameonyesha utayari mkubwa wa kujifunza na kuendana na mfumo mpya, huku kikosi hicho kikitarajiwa kufanya mazoezi ya mwisho leo kukamilisha maandalizi yake.

Hata hivyo, Yanga itapaswa kuwa makini dhidi ya Polisi Tanzania, ambayo ni miongoni mwa timu hatari katika matumizi ya mipira ya kutenga msimu huu.

Kwa mujibu wa takwimu za Ligi Kuu ya NBC, Polisi Tanzania imefunga mabao sita kupitia mipira ya kutenga, ikishika nafasi ya pili nyuma ya Simba yenye mabao manane, huku Yanga ikiwa na mabao matatu katika eneo hilo.

Mchezo huo utakuwa fursa kwa Yanga kuonyesha matunda ya maandalizi yaliyofanyika Zanzibar pamoja na mbinu mpya za benchi lake la ufundi.

Pazia la mchezo huo litafunguliwa saa 10:00 jioni, huku Wananchi wakilenga kuondoka Moshi na pointi zote tatu muhimu katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC.

More Stories

Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
5h ago
READ MORE β†’
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
11h ago
READ MORE β†’
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
11h ago
READ MORE β†’
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
14h ago
READ MORE β†’
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
14h ago
READ MORE β†’
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
15h ago
READ MORE β†’
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
16h ago
READ MORE β†’
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
17h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
19h ago
READ MORE β†’