Yanga yatangaza viingilio na mfumo wa tiketi kwa mchezo dhidi ya MC Alger

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
26m ago
Yanga yatangaza viingilio na mfumo wa tiketi kwa mchezo dhidi ya MC Alger

Afisa Habari na Mawasiliano wa Young Africans, Ali Kamwe, ametangaza viingilio vya mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya MC Alger utakaochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Amaan Complex, Zanzibar.

Kamwe amesema kikosi cha Yanga tayari kimeanza safari kuelekea Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo, huku akitaja viingilio kuwa vitakuwa Sh 5,000 kwa majukwaa ya Saa na Obit, Sh 10,000 kwa Jukwaa la Urusi, Sh 20,000 kwa Wings za pande zote mbili na Sh 30,000 kwa VIP.

Aidha, amesema tiketi za VVIP hazitauzwa kwa kuwa eneo hilo limetengwa kwa ajili ya wageni maalumu watakaohudhuria mchezo huo.

Katika hatua nyingine, Yanga imetangaza kutumia mfumo wa Lipa Finance Tiketi kurahisisha upatikanaji wa tiketi kwa mashabiki wake. Mashabiki wanaweza kukata tiketi kupitia simu janja au simu za kawaida kwa kubonyeza '*149*46*11#' na kufuata maelekezo yatakayoonekana.

Pia, tiketi zitapatikana kupitia tovuti ya Lipa Yanga kwa kutembelea lipayanga.tiketi.tz. Hatua hiyo inalenga kuwapa mashabiki urahisi wa kupata tiketi zao mapema na kujipanga kwenda kuishangilia timu yao katika mchezo huo muhimu visiwani Zanzibar.

More Stories

Kipigo cha Pyramids chaivuruga Al Ahly, yafukuza kocha, wachezaji kukatwa mishahara
Kipigo cha Pyramids chaivuruga Al Ahly, yafukuza kocha, wachezaji kukatwa mishahara
39m ago
READ MORE β†’
Mechi ya Galatasaray na Aston Villa kuwa mashakani baada ya simba kuonekana karibu na uwanja
Mechi ya Galatasaray na Aston Villa kuwa mashakani baada ya simba kuonekana karibu na uwanja
1h ago
READ MORE β†’
Al Ahly yamfuta kazi kocha wake baada ya kipigo dhidi ya Pyramids
Al Ahly yamfuta kazi kocha wake baada ya kipigo dhidi ya Pyramids
3h ago
READ MORE β†’
Kocha wa zamani Yanga aanza majukumu mapya Afrika Kusini
Kocha wa zamani Yanga aanza majukumu mapya Afrika Kusini
19h ago
READ MORE β†’
Mourinho anaamini Bernado Silva akistaafu ataiongoza Benfica
Mourinho anaamini Bernado Silva akistaafu ataiongoza Benfica
19h ago
READ MORE β†’
MC Alger watimua kocha siku chache kabla ya kukutana na Yanga CAFCL
MC Alger watimua kocha siku chache kabla ya kukutana na Yanga CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Kocha Simba ashitukia jambo, kuongeza dozi kukabiliana na ushindani
Kocha Simba ashitukia jambo, kuongeza dozi kukabiliana na ushindani
20h ago
READ MORE β†’
Hatma ya Afcon 2025 kufahamika Jumanne
Hatma ya Afcon 2025 kufahamika Jumanne
20h ago
READ MORE β†’
Pochettino aanza kwa kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Liverpool
Pochettino aanza kwa kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Liverpool
1d ago
READ MORE β†’
Arsenal kupata pigo baada ya David Raya kuumia, vipimo zaidi kubaini hali yake
Arsenal kupata pigo baada ya David Raya kuumia, vipimo zaidi kubaini hali yake
1d ago
READ MORE β†’