Mwamuzi Abdulaaziz Bouh kutoka Mauritania ndiye atakayesimamia mchezo kati ya Simba SC na Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Bouh amekuwa akionekana mara kwa mara katika mechi za mashindano ya CAF akiwa kama mwamuzi wa akiba (Fourth Official), mara nyingi akifanya kazi pamoja na mwamuzi mwenzake Beida Dahane.
Katika kumbukumbu zake zinazohusisha Simba SC, Bouh alikuwa Fourth Official katika michezo miwili muhimu msimu wa 2024/25. Mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch FC na fainali dhidi ya RS Berkane iliyochezwa Zanzibar.
Safari hii, Bouh anapewa jukumu la kuwa mwamuzi mkuu katika pambano hilo dhidi ya Orlando Pirates.