Ahmed Ally atoa wito kwa Wanasimba: uchaguzi tuweke pembeni, nguvu zielekezwe kwa Orlando

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
•
13m ago
Ahmed Ally atoa wito kwa Wanasimba: uchaguzi tuweke pembeni, nguvu zielekezwe kwa Orlando

Msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally, amewataka Wanasimba kuweka pembeni tofauti zinazotokana na mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo na kuelekeza nguvu zao katika mchezo dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Ahmed Ally amesisitiza kuwa uchaguzi bado upo na umepangwa kufanyika mwakani, hivyo mashabiki wanapaswa kuacha kwa muda mijadala inayohusu uchaguzi na kuungana kuiunga mkono timu. Amesema: “Uchaguzi upo tu. Tukipoteza mechi ya Orlando tutakuwa na hali mbaya, uchaguzi ni mwakani, kilicho karibu ni mechi ya Orlando, tuweke nguvu hapo.”

Aidha, Ally ameeleza kutoridhishwa na kushuka kwa Simba katika viwango vya klabu bora Afrika, kutoka nafasi ya tano hadi ya 11. Kwa mujibu wa takwimu za CAF za msimu wa 2026/27.

Amesisitiza kuwa malengo ya Simba msimu huu si kushiriki tu michuano ya Afrika, bali kuvuka hatua ya makundi na kupambana kufika robo fainali na nusu fainali ambapo mafanikio hayo yanahitaji umoja wa viongozi, wachezaji na mashabiki, badala ya kuendelea kugawanyika katika makundi yanayotokana na uchaguzi.

More Stories

"Orlando apende, asipende atapasuka" Ahmed Ally
"Orlando apende, asipende atapasuka" Ahmed Ally
26m ago
READ MORE →
Huyu hapa pilato wa mechi kati ya simba dhidi ya Orlando Pirates
Huyu hapa pilato wa mechi kati ya simba dhidi ya Orlando Pirates
1h ago
READ MORE →
Kisa Musiala, Kimmich aukosoa uongozi wa Bayern munich
Kisa Musiala, Kimmich aukosoa uongozi wa Bayern munich
2h ago
READ MORE →
Orlando Pirates yawasili Dar es Salaam kuikabili Simba SC
Orlando Pirates yawasili Dar es Salaam kuikabili Simba SC
3h ago
READ MORE →
Al Ahly yaanza upya: Benchi jipya la ufundi laidhinishwa, baadhi ya wachezaji kuuzwa
Al Ahly yaanza upya: Benchi jipya la ufundi laidhinishwa, baadhi ya wachezaji kuuzwa
3h ago
READ MORE →
Azam Fc vs Al Ahly Tripoli, hapatoshi Zanzibar
Azam Fc vs Al Ahly Tripoli, hapatoshi Zanzibar
3h ago
READ MORE →
Yanga yapewa mwamuzi Ambongile Tom mchezo dhidi ya MC Alger
Yanga yapewa mwamuzi Ambongile Tom mchezo dhidi ya MC Alger
3h ago
READ MORE →
Pirates yawasili Dar mapema tayari kuikabili Simba
Pirates yawasili Dar mapema tayari kuikabili Simba
3h ago
READ MORE →
UCL: Liverpool yang’ara, Bayern yapigwa huku PSG na Man United wakiambulia sare
UCL: Liverpool yang’ara, Bayern yapigwa huku PSG na Man United wakiambulia sare
13h ago
READ MORE →
Ofisi za CAF zazinduliwa rasmi Dar es salaam
Ofisi za CAF zazinduliwa rasmi Dar es salaam
20h ago
READ MORE →