Alama tatu ndio lengo letu dhidi ya Mc Alger: Fadlu Davids

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
21m ago
Alama tatu ndio lengo letu dhidi ya Mc Alger: Fadlu Davids

Kocha mkuu wa Yanga SC, Fadlu Davids, amesema kikosi chake kinalenga kuanza kwa ushindi kampeni ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kitakapokutana na MC Alger ya Algeria, akisisitiza kuwa dhamira yao ni kuondoka na pointi zote tatu katika mchezo huo.

Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Novemba 28, 2026, saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Fadlu amesema wanatambua ubora wa wapinzani wao, lakini pia wana imani na uwezo wa kikosi chao kupata matokeo mazuri.

Kocha huyo amesema Yanga ina matarajio makubwa katika mashindano hayo na ndoto ya kufika mbali, lakini kwa sasa kipaumbele ni mchezo wa kwanza. Ameeleza kuwa kucheza nyumbani katika ufunguzi wa hatua ya makundi ni fursa muhimu ambayo wanapaswa kuitumia vizuri.

“Lengo letu ni kupata pointi zote tatu,” amesema Fadlu, akisisitiza kuwa Yanga inahitaji kuingia uwanjani kwa mtazamo chanya, kucheza soka lake la kushambulia na kupambana kuhakikisha inaanza safari hiyo kwa ushindi.

Mchezo huo pia utakuwa mtihani wa kwanza wa Fadlu katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika tangu achukue mikoba ya ukocha wa Yanga kufuatia kuondoka kwa Manqoba.

More Stories

Tumepata wiki moja pekee, lakini tumejipanga kimwili na kiakili kuivaa MC Alger: Fadlu Davids
Tumepata wiki moja pekee, lakini tumejipanga kimwili na kiakili kuivaa MC Alger: Fadlu Davids
6m ago
READ MORE β†’
EPL: Mechi kuendelea leo, Chelsea yakutana na Nottingham Forest
EPL: Mechi kuendelea leo, Chelsea yakutana na Nottingham Forest
1h ago
READ MORE β†’
Kimoto apania kuwaadhibu waajiri wake wa zamani, AS Maniema Union
Kimoto apania kuwaadhibu waajiri wake wa zamani, AS Maniema Union
1h ago
READ MORE β†’
Azam FC kuanza kazi leo na Mayele, Amaan stadium itawaka moto
Azam FC kuanza kazi leo na Mayele, Amaan stadium itawaka moto
4h ago
READ MORE β†’
Kocha Orlando Pirates atoa maua yake kwa Steve Barker wa Simba: 'Afrika Kusini ijivunie'
Kocha Orlando Pirates atoa maua yake kwa Steve Barker wa Simba: 'Afrika Kusini ijivunie'
5h ago
READ MORE β†’
Ahmed Ally atoa wito kwa Wanasimba: uchaguzi tuweke pembeni, nguvu zielekezwe kwa Orlando
Ahmed Ally atoa wito kwa Wanasimba: uchaguzi tuweke pembeni, nguvu zielekezwe kwa Orlando
22h ago
READ MORE β†’
Orlando apende, asipende atapasuka - Ahmed Ally
Orlando apende, asipende atapasuka - Ahmed Ally
22h ago
READ MORE β†’
Huyu hapa pilato wa mechi kati ya Simba dhidi ya Orlando Pirates
Huyu hapa pilato wa mechi kati ya Simba dhidi ya Orlando Pirates
23h ago
READ MORE β†’
Kisa Musiala, Kimmich aukosoa uongozi wa Bayern munich
Kisa Musiala, Kimmich aukosoa uongozi wa Bayern munich
1d ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasili Dar es Salaam kuikabili Simba SC
Orlando Pirates yawasili Dar es Salaam kuikabili Simba SC
1d ago
READ MORE β†’