Tumepata wiki moja pekee, lakini tumejipanga kimwili na kiakili kuivaa MC Alger: Fadlu Davids

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
17m ago
Tumepata wiki moja pekee, lakini tumejipanga kimwili na kiakili kuivaa MC Alger: Fadlu Davids

Kocha mkuu wa Young Africans (Yanga), Fadlu Davids, amesema kwa mara ya kwanza tangu kurejea kwa wachezaji kutoka kwenye majukumu ya timu za taifa amepata nafasi ya kufanya kazi na kikosi kizima, akieleza kuwa wiki hii itakuwa muhimu katika maandalizi ya mchezo dhidi ya MC Alger ya Algeria.

Kocha huyo amesema benchi la ufundi limetenga muda huo kwa mazoezi ya uwanjani, uchambuzi wa video na maandalizi ya kiufundi ili kuhakikisha wachezaji wanakuwa tayari kimwili, kiakili na kisaikolojia kuelekea mchezo huo wa ufunguzi wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumzia maandalizi hayo, Fadlu amesema wanachambua kwa makini wapinzani wao, ikiwemo mechi yao ya karibuni dhidi ya JS Kabylie. Ameeleza kuwa mabadiliko ya benchi la ufundi la MC Alger yameleta baadhi ya tofauti za kiufundi ambazo Yanga inapaswa kuzifahamu, lakini akasisitiza kuwa kipaumbele chao ni kujiandaa vizuri na kuboresha maeneo yao ya ushambuliaji kabla ya kukutana na Waarabu hao Novemba 28, 2026, katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

More Stories

Alama tatu ndio lengo letu dhidi ya Mc Alger: Fadlu Davids
Alama tatu ndio lengo letu dhidi ya Mc Alger: Fadlu Davids
31m ago
READ MORE β†’
EPL: Mechi kuendelea leo, Chelsea yakutana na Nottingham Forest
EPL: Mechi kuendelea leo, Chelsea yakutana na Nottingham Forest
1h ago
READ MORE β†’
Kimoto apania kuwaadhibu waajiri wake wa zamani, AS Maniema Union
Kimoto apania kuwaadhibu waajiri wake wa zamani, AS Maniema Union
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC kuanza kazi leo na Mayele, Amaan stadium itawaka moto
Azam FC kuanza kazi leo na Mayele, Amaan stadium itawaka moto
4h ago
READ MORE β†’
Kocha Orlando Pirates atoa maua yake kwa Steve Barker wa Simba: 'Afrika Kusini ijivunie'
Kocha Orlando Pirates atoa maua yake kwa Steve Barker wa Simba: 'Afrika Kusini ijivunie'
5h ago
READ MORE β†’
Ahmed Ally atoa wito kwa Wanasimba: uchaguzi tuweke pembeni, nguvu zielekezwe kwa Orlando
Ahmed Ally atoa wito kwa Wanasimba: uchaguzi tuweke pembeni, nguvu zielekezwe kwa Orlando
22h ago
READ MORE β†’
Orlando apende, asipende atapasuka - Ahmed Ally
Orlando apende, asipende atapasuka - Ahmed Ally
22h ago
READ MORE β†’
Huyu hapa pilato wa mechi kati ya Simba dhidi ya Orlando Pirates
Huyu hapa pilato wa mechi kati ya Simba dhidi ya Orlando Pirates
23h ago
READ MORE β†’
Kisa Musiala, Kimmich aukosoa uongozi wa Bayern munich
Kisa Musiala, Kimmich aukosoa uongozi wa Bayern munich
1d ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasili Dar es Salaam kuikabili Simba SC
Orlando Pirates yawasili Dar es Salaam kuikabili Simba SC
1d ago
READ MORE β†’