Young Africans (Yanga SC) imeanza vibaya kampeni yake ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya MC Alger ya Algeria.
Bao pekee la MC Alger limefungwa na Bayazid dakika ya 90, likiipa timu hiyo ushindi muhimu katika mchezo uliopigwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuanza safari ya kusaka nafasi ya kufuzu hatua inayofuata kwa kupoteza pointi zote tatu katika mchezo wake wa kwanza.