Kocha Juma Mwambusi ataiongoza Yanga mpaka mwishoni mwa msimu, uongozi wa Yanga umethibitisha
Mwambusi alirejeshwa wiki iliyopita baada ya Yanga kuvunja benchi kla ufundi lililokuwa likiongozwa na kocha Cedric Kaze
Wakati mchakato wa kusaka kocha mpya ukiendelea, Yanga imemkabidhi Mwambusi aiongoze timu hadi mwishoni mwa msimu
Ni uamuzi ambao ulikuwa wa lazima kwa uongozi kuchukua
Mechi zilizobaki kukamilisha msimu wa VPL ni 11 tu, kuleta kocha mpya kipindi hiki ingewachanganya zaidi wachezaji
Mwambusi anaifahamu vizuri Yanga kwani amekuwa na wachezaji tangu mwanzoni mwa msimu, hivyo itakuwa rahisi kwake kuendeleza pale alipoishia Kaze
Aidha kocha mpya atakuwa na nafasi ya kukisoma kikosi katika michezo iliyobaki ili aweze kufanya marekebisho stahili kwa ajili ya msimu ujao
Ki ukweli muda uliobaki sasa kuelekea mwisho wa msimu hautoshi kwa kocha yeyote mgeni kuleta athari chanya ndani ya kikosi