Meneja wa Metacha Mnata, mlinda lango wa Yanga, Jemedari Said amekanusha taarifa inayoenezwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Mteja wake
Jemedari amesema taarifa hizo zipuuzwe, Metacha ni mchezaji halali wa Yanga na bado ana mkataba na mabingwa hao wa kihistoria
"Metacha Mnata ni mchezaji wa Yanga SC mwenye mkataba, kusema kwamba amesajiliwa na Simba Sc wakati sio kweli ni kuikosea heshima Simba pamoja na mchezaji"
"Simba inasajili vipi mchezaji mwenye mkataba bila Klabu yake kujua! Andiko limelenga sio tu kumchafua mchezaji na kumgombanisha na Klabu yake ambayo anaitumikia kwa uaminifu mkubwa, lakini pia linaichafua Simba kwamba inasajili bila kufuata utaratibu kitu ambacho ni hatari sana"
"Kuna taratibu za usajili ambazo zinafahamika na zinapaswa kufatwa. Andiko hili la kichochezi linaweza kuzua mgogoro kati ya Klabu na mchezaji, lakini hata kati ya klabu hizi kubwa mbili
"Leo tunatoa onyo kwa uongo huu kwa waliohusika kutunga na kusambaza, siku za mbele tutachukua hatua zaidi.
"Mitandao ina sheria na kanuni zake ambazo tunapaswa kuzifata. Mtu unaposema una uhakika inafaa kuwa una hakika kweli na si vinginevyo ikibidi ambatanisha na ushahidi kinyume chake unakua uzushi na kuchafuliana majina kitu ambacho hakivumiliki," amesema