Mwambusi akomaa na 'fitnes' ya wachezaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Mar 2021
Mwambusi akomaa na 'fitnes' ya wachezaji

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Juma Mwambusi anapambana kurejesha utimamu wa wachezaji wake kabla ya kurejea kwa mikiki mikiki ya ligi kuu na michuano ya kombe la FA

Baada ya kutangazwa kuiongoza Yanga mpaka mwishoni mwa msimu, Mwambusi aliandaa program maalum ya mazoezi ambayo iliwataka wachezaji kufanya mazoezi mara mbili kwa siku isipokuwa siku ya Ijumaa ambayo wanafanya mara moja

Hata hivyo kutokana na kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano hayati Dk John Magufuli, Yanga imesitisha mazoezi kwa muda wakati huu wa maombolezo timu ikitarajiwa kurejea kambini Ijumaa

Mwambusi amesema alibaini madhaifu ya baadhi wachezaji kutokuwa fiti, hivyo aliandaa program ambayo itawarejesha katika ubora wao

"Tumeanza na mazoezi ya kutengeneza 'fitness' ya wachezaji. Tunakwenda vizuri, naamini tutakaa sawa baada ya muda mfupi," alisema Mwambusi

Mwambusi anafahamika kwa umahiri wake katika kujenga utimamu wa wachezaji

Wengi wanakikumbuka kile kikosi cha Mbeya City alichokipandisha daraja msimu wa 2013/14 na kutoa ushindani mkali katika msimu wake wa kwanza ligi kuu akimaliza katika nafasi ya tatu

Msimu uliofuata akajiunga na Yanga akiwa kocha msaidizi wakati huo Yanga ikinolewa na Hans van Pluijm

Alichukua nafasi ya Charles Boniface Mkwasa ambaye aliteuliwa kuinoa timu ya Taifa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’