Yanga ya Mwambusi haina 'kuremba'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Mar 2021
Yanga ya Mwambusi haina 'kuremba'

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Juma Mwambusi ameweka wazi aina ya soka ambalo anataka kikosi chake kicheze

Kocha huyo aliyewahi kuinoa klabu ya Mbeya City kwa mafanikio makubwa, amesema anaiandaa timu yake kuchezaΒ  'direct football'

Wakati wa kocha Cedric Kaze, Yanga ilitumia mfumo wa tiki-taka ambao wachezaji wanatengeneza nafasi wakitokea nyuma kwa kupasiana

Mwambusi amebainisha kutakuwa na mabadiliko ya mfumo huo kwani atahitaji timu itengeneza nafasi nyingi za mabao hivyo watahitaji kuwa katika lango la wapinzani wao mara kwa mara

"Tunakwenda vizuri na program ya mazoezi, Tunafanya mazoezi ya ufiti na mbinu, tunakwenda vizuri, wachezaji wamejitoa, sina shaka kwamba Ligi itakapoendelea tutazidi kuwa bora zaidi"

"Sisi tutacheza direct football, tutahitaji kushambulia sana ili tufunge mabao," alisema Mwambusi

Vinara hao wa ligi, wanapaswa wafanye vizuri katika michezo 11 iliyobaki ili waweze kutimiza lengo la kutwaa ubingwa msimu huu

Mechi zilizobaki kumaliza msimu zinatarajiwa kuwa na ushindani mkali, Mwambusi amewaongezea wachezaji wake dozi ya mazoezi ili kuhakikisha wanakuwa fiti na tayari kwa mapambano

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’