Wakati alipotembelea klabu ya Yanga wiki iliyopita, Mkurugenzi Mkuu wa tathmini, Usajili wa Wachezaji na Maendeleo ya klabu ya Kaizer Chiefs, Walter Steenbok alieleza jinsi gani walistaajabu kusikia Mukoko Tonombe na Tusila Kisinda wamesajiliwa Yanga
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amedokeza kuwa bosi huyo wa kitengo cha usajili Kaizer Chiefs alitaka kujua mbinu za Scouting za Yanga kwani wao Kaizer Chiefs waliwafuatilia nyota hao wakiwa AS Vita kwa miaka miwili mfululizo
"Tuliwafutilia Mukoko na Tusila wakiwa AS Vita, tulipoenda tena tukaambiwa wamechukuliwa na Yanga, nilitaka kujua mbinu zenu za Scouting, japo Yanga hamna scouting team lakini niwapongeze kwa jicho lenu kwa Wachezaji hawa ambao hata sisi tuliwaona," alisema Steenbok.
Hii maana yake ni kwamba Eng. Hersi Said na kamati ya Ufundi walikuwa na jicho la tatu lililowazidi kete Kaizer Chiefs ambo walikuwa na Timu kubwa na mfumo wa kisasa wa Scouting ya Wachezaji
Nugaz amebainisha kuwa hakukuwa na nia yoyote ya Kaizer Chiefs kumchukua Mukoko wala Tuisila