Kumekuwepo na fungia fungia ya viongozi wengi wa vilabu na hata vyama vya Soka ambao hawaendani na falsafa ya akina viongozi wa TFF Rais Wallace Karia na Katibu Mkuu Wilfred Kidau
Katika kipindi cha miaka mitano watu wengi wamejikuta hatiani na kufungiwa kuto kushiriki Michezo pasipo na hata Sababu
Mgombea wa chama cha Soka mkoa wa Tabora TAREFA ,DICKSON MLIMUKA alifungiwa na KAMATI YA maadili akiwa na mwenzake Stella Kwa kosa la kushiriki kikao chama chama cha Soka Wilaya ya Urambo..Wakati MLIMUKA alipewa idhini hiyo na sekreteriat ya chama cha Soka mkoa wa Tabora kuwa aende Urambo kama observer tuu...
MWENYEKITI wa chama cha Soka mkoa wa Shinyanga Bwana Benister Rogora alifungiwa na KAMATI YA maadili ya T.F.F kuto kujihusisha na Soka.
MWENYEKITI wa chama cha Soka mkoa wa Songwe Bwana Erick Ambakisye naye alifungiwa kisa Waamuzi hawakulipwa Kwa Wakati akatengenezewa Shahidi Faki akapigwa nyundo ..
Katibu wa chama cha Soka Tabora Athuman Kilundumya alifungiwa kisa pesa za mkutano mkuu Arusha ,Wakati Karia katika Uongozi wa kina Malinzi vipo vikao vingi haku hudhiria na posho alikula.
Viongozi chama cha Soka mkoa wa Pwani walifungiwa kisa nyaraka za T.F.F kuziweka hadharani
Viongozi wa Lipuli walifungiwa kisa walidai fedha zao za mshindi WA pili wa mashindano ya FA.
Hassan Bumbuli alifungiwa Kwa hira tuu za Usimbaism kisa alikuwa akiwasema Simba Sana
Zahera alitafutiwa kanuni yake baada ya kutoka katika kufundisha kanuni ikafutwa na walifungia Sana.
Elias Mwanjala walimfungia kupitia sakata la Morrison
Kiongozi wa Geita Gold alifungiwa kisa kuuliza kwanini mechi za play off zinaonyeshwa live na Azam Wakati wao hawanufaiki.
Leo hii wamemalizia kumfungia MWAKALEBELA
T.F.F Ni tasisi nanyi mtaondoka, mbona hamjikosoi wenyewe Kwa mambo ya hovyo...???
Mmefanya vibaya timu zote za Taifa mbona hamjahukumiwa?
credit : @abdulsportstz