Mwambusi ashindwe mwenyewe, timu imekamilika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Apr 2021
Mwambusi ashindwe mwenyewe, timu imekamilika

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Juma Mwambusi atakuwa na wakati mzuri pale ligi itakaporejea kwani asilimia 99 ya wachezaji wake wako fiti

Kwa sasa mchezaji pekee anayekosekana kikosini ni kiungo Mapinduzi Balama ambaye anafanya program ya peke yake ya mazoezi

Juzi wachezaji waliokuwa na majukumu ya Kimataifa Saido Ntibazonkiza na Haruna Niyonzima walirejea wakati Mukoko alirejea mapema zaidi

Tangu mwezi Januari 2021 baada ya michuano ya kombe la Mapinduzi, Yanga iliandamwa na majeruhi kwa wachezaji wake muhimu Yacouba Songne, Michael Sarpong, Saido Ntibazonkiza na Dickson Job ambaye bado hajacheza hata mechi moja tangu aliposajiliwa dirisha dogo

Job sasa amepona tayari kuwapa changamoto kina Lamine Moro na Bakari Nondo Mwamnyeto ambao wamekuwa chaguo la kwanza kwenye safu ya ulinzi

Lakini pia kurejea kwa Ntibazonkiza ni faida kubwa kwa Mwambusi. Kama atamtumia vizuri nyota huyu kutoka Burundi ataongeza makali katika safu ya ushambuliaji

Haruna Niyonzima alikuwa na wakati mzuri sana wakati akiitumikia timu ya Taifa ya Rwanda. Alionyesha kiwango kizuri sana katika michezo dhidi ya Msumbiji na Cameroon

Nae anaweza kuwa na mchango mkubwa kuelekea mechi za kukamilisha msimu

Mwambusi ataongoza mchezo wake wa kwanza akiwa Kaimu Kocha Mkuu dhidi ya KMC Jumamosi ijayo pale uwanja wa Benjamin Mkapa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’