Baada ya klabu ya Chippa United kumtangaza Luc Eymael aliyekuwa kocha wa Yanga kuwa Mkurugenzi wake wa ufundi, bado matukio yake ya ubaguzi aliyofanya Tanzania yanaendelea kumuandama kwani kumekuwa na shinikizo kubwa kuitaka Chippa United iachane nae
Baada ya kutimuliwa na Yanga, miezi minne iliyopita aliajiriwa na Klabu hiyo lakini akatimuliwa baada ya Chama cha soka cha Afrika Kusini kulalamika kuhusu masuala yake ya ubaguzi aliyofanya Tanzania
Baadae Eymael alikata rufaa FIFA na Shirikisho hilo la soka Duniani 'kumsafisha' na tuhuma zote zilizokuwa zikimkabili
Juzi klabu ya Chippa United ikamtangaza kuwa Mkurugenzi wao wa ufundi lakini Chama cha Upinzani Afrika Kusini kinachoongozwa na Julius Malema kimetoa tamko kuitaka Chippa United iachane na kocha huyo mbaguzi mara moja au la watahakikisha hafanyi kazi katika ardhi ya Afrika Kusini
Kwa hakika huyu mwamba atajutia kitendo chake cha kibaguzi alichofanya dhidi ya mashabiki wa Yanga
Makocha aina ya Eymael huko Ulaya ni 'vilaza' wanang'ang'ania kuja Afrika kwa kuwa huku ndiko wanapata 'mkate wao' wa kila siku
Si arudi kwao Ubelgiji akasake timu huko?