Hawa hapa nyota watakaoikosa KMC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Apr 2021
Hawa hapa nyota watakaoikosa KMC

Kaimu Kocha MKuu wa Yanga Juma Mwambusi amebainisha kuwa nyota wake watano watakosekana kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam

Mwambusi amesema pamoja na Mapinduzi Balama, wachezaji Yassin Mustafa, Farid Mussa na Haruna Niyonzima watakosekana kutokana na sababu mbalimbali

Yassin ni mgonjwa wakati Farid nae amerejea siku chache zilizopita baada ya kupona Malaria

Aidha Niyonzima hakupata muda wa kutosha kufanya mazoezi na wenzake baada ya kuchelewa kuingia kambini

Niyonzima alikuwa Rwanda ambako alikuwa akikabiliwa na majukumu ya timu za Taifa

Carlos Carlinhos anatumikia adhabu ya kadi nyekundu, huu ukiwa mchezo wake wa mwisho kukosa kabla ya kurejea dimbani

Aidha kocha Mwambusi amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kuiunga mkono timu yao

Amesema wampania kuondoka na alama zote tatu katika mchezo huo ambao wao watakuwa uwanja wa nyumbani

"Tunacheza tukiwa nyumbani, Wanayanga wanatarajia kupata matokeo mazuri, tutapamabana kupata pointi tatu muhimu na hilo ndiyo jambo muhimu," alisema

Mwmabusi amesema kesho watacheza kwa mfumo wa kushambulia zaidi huku wakichukua tahadhari dhidi ya wapinzani wao KMC ambao ni moja ya timu bora kwenye ligi msimu huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’