Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro ambaye amewahi kuwa msemaji wa klabu ya Yanga, amesema wachezaji wanapaswa kufahamu ukubwa wa klabu ya Yanga
Muro mmoja wa wadau wakubwa wa Yanga, ametoa maoni yake baada ya vinara hao wa ligi kuu kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya KMC katika mchezo uliopigwa mwishoni mwa wiki
Huo ulikuwa mchezo wa tano Yanga inashindwa kuibuka na ushindi katika michezo saba waliyocheza tangu kuanza kwa duru ya pili
Muro amesema mchezaji ukisajiliwa Yanga, fahamu kuwa una deni kubwa kwani umesajiliwa na klabu kubwa na yenye historia ya kipekee hapa Tanzania
Hivyo ni lazima ufahamu ukubwa huo na heshima ya kucheza Yanga
"Wachezaji wa Yanga wanatakiwa kufahamu jambo moja. Yanga ni kubwa sana na mpaka umesajiliwa ujue unatakiwa ufanye kitu cha ziada"
"Sio kucheza cheza tu, sisi sio timu ya kutoka sare na KMC kirahisi rahisi tu," alisema Muro
Wananchi bado wanamkumbuka Muro kwa 'amsha-amsha' zake wakati akiwa Afisa Habari na Msemaji wa Yanga