Napenda Yanga isonge mbele - GSM

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Apr 2021
Napenda Yanga isonge mbele - GSM

Rais wa makampuni ya GSM, Galib Said Mohammed 'GSM' amesema uwekezaji wake ndani ya klabu ya Yanga lengo kuu ni kuona timu hiyo inaondoka katika changamoto za kiuchumi na kuweza kujitegemea

Ghalib amekuwa mtu muhimu sana kwa Yanga tangu msimu uliopita, kampuni yake ikihusika katika usimamizi wa timu pamoja na kuchukua jukumu la kusimamia mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji

GSM pia imeingia makubaliano na Yanga kusimamia mauzo ya jezi pamoja na bidhaa nyingine zenye nembo ya Yanga

Ghalib amebainisha kuwa hakuna faida kubwa anayoipata Yanga lakini yote anayofanya ni kwa ajili ya mapenzi yake kwa Yanga

"Ukija na wazo la kupata faida kwenye timu zetu hizi unajidanganya, tunasaidia hizi timu kwa sababu tunazipenda. Ndio maana tumewaleta La Liga ili kujenga mfumo imara utakaokuwa na manufaa huko mbeleni," alisema Ghalib katika mahojiano ya ana kwa ana na Mwanahabari Privaldinho

Aidha Ghalib amewaalika Wawekezaji wengine wenye nia ya kuisaidia Yanga wajitokeze ili waunganishe nguvu kutengeneza taasisi imara

"Nimezisikia taarifa za Manji (Yusufu) kutaka kurudi Yanga, binafsi nimefarijika sana, kama akirudi, ujio wake utakuwa msaada mkubwa kwa Yanga. Sio Manji tu, yeyote mwenye nia ya dhati ya kuisaidia Yanga, aje tuungane kwa pamoja kwani mshikamano huleta maendeleo maradufu"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’