Leo Yanga itashuka katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Biashara United katika mchezo unaotarajiwa kupigwa kuanzia saa moja usiku
Kuelekea mchezo huo, mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kwani amewaandalia zawadi
Nchimbi amekuwa na changamoto ya kuzifumania nyavu kwa muda mrefu, msimu huu akiwa hajafanikiwa kutumbukiza bao kambani
Mwenyewe amelizungumzia hilo, akikiri kuwa ni jambo linalomuuza hasa ikizingatiwa nyakati ambazo Yanga imekubwa na uhaba wa mabao kutoka kwa washambuliaji wake
"Ni kweli sijafunga muda mrefu, ni jambo linaloniumiza sana. Naamini wakati wangu wa kuisaidia timu umefika hivyo nawaambia mashabiki waje kwa wingi leo kwani nawaahidi nikipata nafasi nitahakikisha nazitumia kuifungia timu yangu," alisema Nchimbi
Msimu uliopita Nchimbi alifunga mabao sita pamoja na kutoa pasi mbili za mabao
Lakini msimu huu ametoa pasi mbili za mabao lakini akiwa hajaweza kuzifumania nyavu
Leo amepania kufungua akaunti yake ya mabao msimu huu kama kocha Juma Mwambusi atampa nafasi ya kucheza