Yanga yasubiriwa kutambulisha kocha mpya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Apr 2021
Yanga yasubiriwa kutambulisha kocha mpya

Yanga imedhamiria kujisahihisha kwa kupata kocha mapema ambaye ataweza kuiimarisha timu na kuwa na muda wa kutosha kuiandaa pale msimu utakapomalizika

Kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu ujio wa kocha huyo, Wananchi wameaswa kusubiri taarifa rasmi kutoka kwa uongozi

Lakini kwa uhakika kocha mpya atawekwa hadharani mapema kabla ya msimu kumalizika

Awali kulikuwa na tetesi za ujio wa kocha Sebastian Migne, lakini leo zimeibuka tetesi nyingine kuwa Yanga wameachana na mpango wa kumleta Migne na huenda wakamtangaza kocha wa zamani wa Al Merrikh Nasredinne Al Nabi mwenye uraia wa Ubelgiji na Tunisia

Lakini zipo taarifa za ndani kuwa mabosi wa Yanga waliwasiliana na kocha wa AS Vita Florente Ibenge kuona uwezekano wa kumleta nchini

Ibenge anaweza kuachana na AS Vita baada ya timu hiyo kukumbwa na ukata ambao ulipelekea kuuza wachezaji wake muhimu

Wakati alipokuja na AS Vita kucheza na Simba, Ibenge alisema kuwa wachezaji wengi wa Kikongo wanakimbilia Tanzania kwa kuwa timu za Tanzania sasa zina fedha kuliko DR Congo

Ibenge anaweza kuwa kocha sahihi kutua Yanga kutokana na uzoefu wake lakini muhimu zaidi anao ushawishi wa kuwaleta wachezaji wazuri

Pengine ni wakati naye kuelekea kwa Wananchi kujiunga na akina Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe ambao aliidhinisha wasajiliwe na Yanga usajili wa dirisha kubwa Julai mwaka jana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’