Mshambuliaji wa Yanga, raia wa Burkinafaso, Yacouba Songne, amesema atautumia mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC, kuendeleza kasi ya ufungaji ili kusaka kiatu cha ufungaji bora msimu huu
Songne amesema atapambana kuhakikisha anaisaidia timu yake kuibuka na ushindi katika mchezo huo wakati yeye akiweka sawa hesabu zake za kuwania kiatu cha ufungaji bora.
"Tunaendelea vizuri na mazoezi kwaajili ya mchezo ujao, nipo fiti kwaajili ya kuipambania timu yangu pamoja na kutimiza malengo yangu ya kuwania ufungaji bora ambao naamini inawezekana kutokana na ushirikiano ninaoupata kutoka kwa wachezaji wenzangu, amesema
Yanga wataingia katika mchezo huo utakaopigwa Jumapili usiku wakiwa na kumbukumbu nzuri dhidi ya Azam FC baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza bao lililofungwa na Deus Kaseke
Ilikuwa pasi murua kutoka kwa Yacouba ndio ilipelekea Yanga kuondoka na alama zote tatu Chamazi