Hatua za kuhitimisha mchakato wa Mabadiliko

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Apr 2021
Hatua za kuhitimisha mchakato wa Mabadiliko

Anaandika Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM mhandisi Hersi Said;

Mfumo pendekezwa wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu ya YANGA umekamilika rasmi.

Kamati ya mabadiliko chini ya Mwenyekiti wake msomi, ALEX MGONGOLWA ilifanya kazi maridhawa kwa ushauri wa LA LIGA na kukabidhi ripoti yake kwa Mwenyekiti wa klabu, Dr. Mshindo Msolla.

Baada ya hapo, Dr. Msolla kwa mamlaka aliyonayo, aliunda kamati ya mabadiliko ya KATIBA kuendana na mfumo pendekezwa chini ya mwanasheria msomi RAYMOND WAWA.

Kamati hizo mbili zimefanya kazi kubwa sana na nichukue fursa hii binafsi kuwapongeza wanakamati kwa kujitoa kwa ajili ya YANGA bora ya kesho.

Aidha, kilichobaki sasa ni muongozo na baraka za washika dau wa michezo nchini hususan;

1. Wizara yenye dhamana na michezo.
2. Baraza la michezo la Taifa.
3. Fair competition commission - FCC
4. TFF
5. Bodi ya Ligi.

Idara hizo hapo juu na nyinginezo zitatupa MUONGOZO wa SEREKALI
juu ya mabadiliko ya vilabu nchini kwa maslah mapana ya taifa kwa ujumla.

Pia, semina elekezi kwa viongozi wa matawi zitatolewa kwa madhumuni ya kusambaza elimu ya mabadiliko haya na pia kupokea MAONI ya wanachama ili kuyafanya mabadiliko haya kuwa shirikishi na yenye maslah mapana ya klabu yetu.

Mwisho, MKUTANO MKUU wa wanachama utafanyika kupata UAMUZI na BARAKA za wanachama kuelekea MABADILIKO.

Safari rasmi ya utelekelezaji wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji itakuwa imeanza, Inshallah, panapo majaaliwa yake mwenyezi mungu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’