Ni siku nyingine kwa mashabiki wa Yanga kushuhudia burudani kutoka kwa timu yao katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Majira ya saa mbili na robo usiku Wananchi watakabiliana na Azam Fc katika mchezo ambao Yanga inahitaji alama zote tatu ili iweze kurejea katika nafasi yake
Baada ya takribani miezi sita kupita, kwa mara ya kwanza Yanga imeachia nafasi ya uongozi wa ligi kwa watani zao Simba walioshinda mchezo dhidi ya Gwambina Fc jana
Hivyo leo ni ushindi pekee ambao utawarejesha Wananchi kileleni na kuendelea kubaki katika mbio za kuwania ubingwa
Kocha Razak Siwa amesema kwa maandalizi waliyofanya, wana matumaini ya kuondoka na alama zote tatu leo
Kikosi cha Yanga kiko imara, ni wachezaji wawili pekee ambao watakoseka, Mapinduzi Balama na Tuisila Kisinda
Kila la kheri wananchi