Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kutinga Sumbawanga leo tayari kwa mchezo wa kombe la FA (ASFC) hatua ya 16 bora dhidi ya Tanzania Prisons
Mchezo huo utapigwa kesho Ijumaa katika uwanja wa Nelson Mandela
Yanga iliweka kambi ya muda mfupi mkoani Mbeya kujiandaa na mchezo huo ambao Wananchi wanahitaji kushinda ili waweze kutinga robo fainali
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema kikosi kiko tayari kwa mchezo huo
"Tuko tayari kwa ajili ya Mchezo wa kesho dhidi ya Tanzania Prisons kwenye hatua ya 16 Bora ya ASFC ambao tutaucheza kwenye Uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga saa 10 Kamili jioni"
Huu utakuwamchezo wa pili wa kocha Nasreddine Nabi ambaye alipoteza mchezo uliopita dhidi ya Azam Fc
Kwa hakika hatakuwa tayari kuiona timu yake ikipoteza mchezo wa pili mfululizo