'Pre-contract' haitambuliki kwenye sheria za Tanzania - Simon

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
29 Apr 2021
'Pre-contract' haitambuliki kwenye sheria za Tanzania - Simon

Jana Mwanahabari Shaffih Dauda alidai kuwa wachezaji wa Simba Shomari Kapombe na Mohammed Hussein walisaini mikataba ya awali 'pre-contract' na Yanga kuelekea kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria mwishoni mwa msimu

Mwanasheria na Kaimu Katibu Mkuu wa zamani wa Yanga Simon Patrick ametoa ufafanuzi kuhusu kitu kinachoitwa pre-contract na uhalali wake katika sheria za Tanzania

Amewataka Wanahabari kuzingatia misingi ya sheria pale wanapotimiza majukumu yao

"Hapa kwetu waandishi wa habari wenye taaluma zao wamebaki wachache na wameanza kupotezwa na kundi la watu maalufu na wenye wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii ambao wameanza kufanya kazi ya habari kiurahisi sana, hii ni hatari sana kwa taifa"

"Tasnia ya michezo wengi wanaichukulia kimchezomchezo, ndiyo maana ni rahisi sana kwa Waandishi wa Habari za michezo nchini na wamiliki wa Mitandao ya kijamii kuandika habari, tuhuma au kumuhoji mtu ambaye anaweza kutoa shutuma kwa taasisi nyingine bila ushahidi wa wazi, kutukana na kudhihaki taasisi ya michezo"

"Mfano mwingine ni wa ndugu yangu Shaffih Dauda ambaye ameweka wazi kwamba kuna wachezaji wamesaini “Pre-contract” na Yanga walisubiri msimu uishe watambulishwe rasmi. Swali rahisi “sasa kama wamesaini pre-contract tayari imekuwaje wachezaji hao wameongeza mkataba na klabu zao, nini umuhimu wa pre-contract kisheria kama unaweza kusaini na mtu na baadae huyo mtu akaenda kusaini sehemu nyingine? Ina nguvu gani kisheria? Je sheria zetu zinatambua pre-contract kama makubaliano halali au mkataba? Au tunaandika vitu tu kwa ajili ya followers wetu?"

"Elimu ya bure ni kwamba, Tanzania kama nchi inayofata “Common Law Tradition” haitambui Pre-Contract agreement, na hakuna sheria yoyote ya kuweza ku enforce hiyo pre-contract hapa Tanzania, hivyo basi kwakuwa ni kitu ambacho hakitambuliki kwenye sheria zetu hakuna mtu wa kupoteza muda wake kumsainisha mtu kitu kisichokuwa na maana au binding effect mchezaji. Yanga ina viongozi smart sana wenye uwezo mkubwa wa kujua mambo madogo kama haya, kwakuwa ni taasisi ya michezo tusiwachukulie kimchezomchezo pia viongozi"

"Kwenye sheria kuna msemo usemao “kutojua sheria sio kinga ya kutoshtakiwa kwa kutenda kosa” niwashauri wanahabari wote wakongwe na chipukizi kwa muda wenu mkasome vizuri sheria hizi; Media Service Act, 2016, Media Services (Defamation Proceedings) Rules 2019, Electronic & Postal Communications (Radio & Television Broadcasting Content) Regulations 2018 na Electronic & Postal Communications (Online Content) Regulations, 2020, mtanishukuru siku za usoni"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →