Kikosi cha Yanga kinaendelea kujifua Mji wa Avic Towan Kigamboni kujiandaa na mchezo wa dabi dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi, May 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mwamba Saido Ntibazonkiza ni miongoni mwa wachezaji wanaojifua kisawasawa tayari kuwapa burudani Wananchi siku hiyo
Huu utakuwa mchezo wa pili wa dabi kwa Saido ambaye mchezo wake wa kwanza ni ule wa fainali michuano ya kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar
Saido ndiye aliyefunga mkwaju wa mwisho wa penati ambao uliihakikishia Yanga ushindi wa penati 4-3
Huyu ni mchezaji mwenye uzoefu na mechi kubwa, bila shaka siku ya Jumamosi atakuwa chachu ya furaha ya Wananchi baada ya dakika 90
ADVERTISE HERE