Wadau wataka ratiba ya ligi izingatiwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 May 2021
Wadau wataka ratiba ya ligi izingatiwe

Wadau wameishauri TFF na Bodi ya Ligi kuhakikisha wanazingatia ratiba ya mechi za ligi ili usawa uonekane miongoni mw timu zote

Ushiriki wa baadhi ya timu kwenye michuano ya CAF umetumika mara nyingi kuvuruga ratiba ya ligi kuu

Baadhi ya timu mpaka sasa hazijacheza hata mechi za duru ya kwanza wakati ligi inaelekea ukingoni

Katibu Mkuu wa zamani wa TFF Angetile Osiah ni miongoni mwa wadau walioohoji sintofahamu hiyo

Tumeshuhudia kwenye ligi za wenzetu pamoja na timu kuwa na majukumu ya Kimataifa, zinaendelea kucheza mechi zao za ligi

Mfano mzuri ni Kaizer Chiefs ambao keshokutwa Jumamosi watacheza na Simba mechi ya ligi ya mabingwa lakini jana walikuwa uwanjani kucheza mechi ya ligi kuu ya Afrika Kusini

Wapinzani wao Simba mechi waliyopaswa kucheza Jumanne ilifutwa licha ya kuwa wangeweza kucheza mchezo huo na kuondoka siku hiyo hiyo kwenda Afrika Kusini

Utaratibu huu ndio unaopelekea kuwa na mkanganyiko wa ratiba huku tmu nyingine zikirundikiwa mechi nyingi za viporo

Mpaka hii leo Simba hawajacheza mechi yoyote na Namungo msimu huu ambao unaelekea ukingoni

Pia ni hivyo hivyo kwa Namungo Fc, hawajacheza mchezo wowote na Gwambina Fc

Ni aibu kama wasimamizi wa mpira nchini wanaona jambo hili ni sawa kwani halishuhudiwi mahali popote duniani isipokuwa Tanzania

Ukweli ni kwamba utaratibu huu unaweza hata kuzitengenezea timu mazingira ya kupanga matokeo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’