Nabi ataanzia hapa msimu ukimalizika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 May 2021
Nabi ataanzia hapa msimu ukimalizika

Pamoja na kukabiliwa na presha ya kupata matokeo wakati msimu ukiwa unaelekea ukingoni, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ameendelea kukifanya tathmini kikosi chake ili kufanya maboresho msimu ukimalizika

Uongozi wa Yanga ulimleta mapema Nabi ili aweze kufahamu mazingira pamoja na kutathmini kikosi kwa ajili ya maboresho ambayo atayafanya mwishoni mwa msimu

Eneo ambalo kila mmoja anatarajia kuwa na maboresho ni safu ya ushambuliaji

Kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake, Nabi naye amekumbana na changamoto katika eneo hilo

Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Yanga, Dominic Albinius ‘Baba Paroko’ amedokeza kuwa Nabi anapanga kusajili wachezaji wasiopungua watano katika safu ya ushambuliaji

"Kama klabu tunajua wapi pa kuanzia kwa msimu ujao na bahati nzuri ni kwamba kumleta kocha mapema  kumeanza kuleta matunda kwa kocha kuanza kuonyesha anachotaka kwa msimu ujao," Albinus amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

"Mpaka sasa ripoti ya awali ambayo Nabi ametueleza, anataka kuongeza mpaka wachezaji watano katika eneo la ushambuliaji na wengine kuwapisha wapya."

Albinus amesema eneo la ushambuliaji ndio litasimamiwa kwa umakini mkubwa ambapo washambuliaji wa kati mawinga na viungo wa pembeni wataongezwa

"Kocha anasema timu inatengeneza nafasi shida ipo katika kuzitumia kwahiyo lazima tuongeze watu wenye ubora zaidi. Huku kwingine kwa viungo wa pembeni nako anataka mtu mwenye ubora zaidi, kwasasa kama tunamkosa Kisinda (Tuisila) hakuna nguvu nyingine"

"Eneo la kiungo ushambuliaji wa kati nako kuna mtu anahitajika kocha anaona hakuna ubunifu wa kutengeneza nafasi nako tutatafuta mtu muafaka atakayekuwa na ubora wa kutengeneza nafasi eneo hilo," aliongeza Albinus

Msimu huu ulikuwa wa matumaini makubwa kwa wanachama na mashabiki wa Yanga, lakini ni wazi huenda ukamalizika pasipo matarajio ya wengi kufikiwa

Lakini kwa hakika ipo kazi imefanyika, wakati mwingine usajili ni bahati nasibu. Mchezaji anaweza kutamba klabu moja akashindwa kufanya hivyo kwenye klabu nyingine

Nabi ni kocha wa daraja la juu, anafahamu wapi anahitaji kupaboresha ili kutengeneza kikosi imara zaidi

Habari njema ni kuwa, wadhamini GSM wameahidi kutimiza mahitaji yote ya kocha ili msimu ujao Yanga irejee ikiwa imara zaidi ya msimu huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’