Lamine atoa maelezo Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 May 2021
Lamine atoa maelezo Yanga

Uongozi wa klabu ya Yanga leo ulimuhoji nahodha Lamine Moro ambaye anatuhumiwa kwa makosa ya utovu wa nidhamu aliyoyafanya wakati kikosi cha Yanga kikiwa mkoani Mtwara kujiandaa na mchezo dhidi ya Namungo Fc

Lamine alirejeshwa jijini Dar es salaam baada ya kutokea tofauti kati yake ya Kocha Nasreddine Nabi

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji Mfikirwa amesema walimuita Lamine kutoa maelezo yake baada ya sintofahamu iliyotokea Mtwara

"Benchi la Ufundi limelalamika, na kwa nafasi yao walichukua hatua za awali zilizoko kwenye Mamlaka yao, kwa kuwa wamelileta kwa Uongozi, sasa ni muhimu Sana tukamsikiliza mlalamikiwa kisha kutoa maamuzi kama klabu," alisema Haji.

Mfikirwa alisisitiza kuwa suala la Lamine ni la kinidhamu lililoanzia kwenye bechi la ufundi na halihusiani chochote na kuidai klabu, nyota huyo hana deni lolote analodai

"Lamine hadai chochote, hivyo taarifa za kwamba anaidai klabu ni za uzushi na zipuuzwe, suala lake limetokana na masuala ya benchi la ufundi, na tutalitolea taarifa baada ya kamati kukaa na kusikiliza"

Inaelezwa kocha Nabi alimtaka Lamine ambaye ni majeruhi ahudhurie mazoezi kuangalia kile kilichokuwa kinafanyika 

Hata hivyo Lamine alisisitiza kuwa alihitaji kuonana na daktari wake hivyo asingeweza kuhudhuria program hizo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’