Uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa wachezaji watatu kati ya nane wanaokosa mchezo dhidi ya Mwadui Fc leo, wanakabiliwa na makosa ya utovu wa nidhamu
Metacha Mnata na Michael Sarpong wameondolewa kikosini wakiungana na nahodha Lamine Moro wakikabiliwa na makosa ya utovu wa nidhamu

Nyota wengine Yassin Mustafa (majeruhi), Carlinhos (majeruhi), Abdallah Shaibu (majeruhi), Saido Ntibazonkiza (majeruhi) na Haruna Niyonzima (matatizo ya kifamilia)
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amejipambanua kutowahitaji wachezaji watovu wa nidhamu katika kikosi chake
Nyota hawa ni kama wanajiondoa wenyewe kikosini kwani kigezo cha nidhamu kitawahukumu pale dirisha la usajili litakapofunguliwa
ADVERTISE HERE