Mfadhili, Mhisani na Mdhamini wa klabu ya Yanga Ghalib Said Mohammed ambaye pia ni Rais wa Makampuni ya GSM, ameipongeza Azam Media kwa udhamin mnono walioweka kupata haki za Matangazo ya Ligi Kuu kwa kipindi cha miaka 10
Ghalib amesema Azam Media wamekuza thamani ya ligi kuu ya Tanzania Bara pamoja na kuvitendea haki vilabu kwenye mapato
Ghalib ambaye moja ya makampuni yake inasimamia mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji Yanga, amesema Azam Media wamewatendea haki Watanzania kwa kuonyesha karibu asilimia 99% za mechi zote ligi kuu
ADVERTISE HERE