Kimya kingi kina mshindo mkuu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jun 2021
Kimya kingi kina mshindo mkuu

Jana uongozi wa Yanga umedokeza mwenendo wa shauri walilofungua dhidi ya Bernard Morrison

Ni muda mrefu umepita tangu shauri hilo lilipozungumzwa wengi wakiamini ni siasa za viongozi wao kuwatuliza na kuwa hakuna kesi yoyote iliyofunguliwa Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa michezo (CAS)

Shauri la Morrison limewaingiza viongozi wa Yanga matatani. Alifungiwa Afisa Habari Hassan Bumbuli kabla ya Yanga kupambana kumtoa kifungoni

Kisha akafungiwa Makamu Mwenyekiti Fredrick Mwakalebela ambaye mpaka leo bado jitihada za kumtoa kifungoni zinaendelea

Lakini sasa ni uhakika, kesi ipo palepale na ITASIKILIZWA

Ukiangalia barua ya CAS kwenda kwa Yanga na Morrison, imebainisha kuwa mpaka kufikia kesho Jumatano Juni 02, pande zote zinatakiwa kuwa zimewasilisha vielelezo zaidi (kama vipo) au la watatoa hukumu kwa kuzingatia vielelezo walivyopokea awali

Aidha inaonekana Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) walikuwa upande wa Morrison wakiomba kesi hiyo irejeshwe kusikilizwa nchini, CAS wamekataa na kusisitiza wanayo Mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo

Hii ni hatua muhimu sana kwani kila mtu anafahamu hukumu ya awali ilivyokuwa, Yanga isingepata haki kama kesi ingerudishwa kwa watu walewale waliotoa hukumu ya awali

Kuna kila dalili, upo mchezo mchafu umefanyika na pengine Yanga wanaweza kuipata haki waliyonyimwa hapa nyumbani

Kama Yanga watashinda kesi hii, madhara yake yatakuwa makubwa kwa Morrison mwenyewe na hata klabu ya Simba

Kuna fidia, kufungiwa mchezaji, klabu kunyan'ganywa pointi ambazo mchezaji huyo alishiriki na hata kufungiwa kusajili

Na hapa yapaswa kumbukumbu kuwekwa sawa, Yanga haipiganii kumrejesha Morrison, bali wanapigania haki yao waliyonyan'ganywa na TFF

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’