Mshambuliaji wa Horoya Ac Heritier Makambo bado anawakumbuka Wananchi akiamini siku moja anaweza kurejea tena
Yanga ilimuuza Makambo kwenda klabu ya Horoya Ac mwaka juzi
Katika usajili uliopita, GSM walijaribu kumrejesha bila ya mafanikio kwani Horoya walitaka kiasi kikubwa cha fedha ili kumuachia
Makambo amesema kuwa anayakumbuka sana maisha ya Tanzania zaidi anaikumbuka klabu ya Yanga
Msimu wake mmoja na Yanga ulitosha kuthibitisha umahiri wake akifunga mabao 18 ndani ya ligi kuu ya Vodacom
Ana kila sababu ya kuikumbuka Yanga kwani ni klabu iliyomtangaza na kumpa mafanikio
Tangu alipojiunga na Horoya, hana wakati mzuri wa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza
Lakini pia huku kwa Wananchi pia tangu alipoondoka, Yanga imeshindwa kupata mshambuliaji wa kariba yake