Kiungo wa Yanga Mukoko Tonombe jana alikuwa kwenye kikosi kilichoanza cha timu ya Taifa ya DR Congo katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Tunisia uliomalizika kwa wenyeji Tunisia kupata ushindi wa bao 1-0
Hata hivyo Mukoko alishindwa kumaliza mchezo huo baada ya kuumia katika dakika ya 64 nafasi yake ikichukuliwa na Paul Mpoku
Hii ni mara ya pili Mukoko anajumuishwa katika kikosi cha kwanza ukiwa ni mchezo wake wa tatu tangu ajumuishwe timu ya Taifa ya DR Congo

Get well soon..
ADVERTISE HERE