Nabi ataka mechi ya kirafiki kuwapima vijana wake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jun 2021
Nabi ataka mechi ya kirafiki kuwapima vijana wake

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ameuagiza uongozi wa timu hiyo kusaka mechi angalau moja ya kirafiki kukipima kikosi chake kabla ya kurejea kwa mikiki mikiki ya ligi kuu ya Vodacom ngwe ya lala salama

Awali Yanga ilikuwa icheze mechi ya kirafiki dhidi ya African Lyon juzi Jumapili lakini mchezo huo ulifutwa na uongozi wa Yanga kwa kile walichokieleza kuwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji Mfikirwa amesema wanaangalia uwezekano wa kupata timu ya Ligi Kuu kujipima nayo

"Ni kweli kocha amefikisha maombi ya kuhitaji mechi za kirafiki, kulingana na timu nyingi za Ligi Daraja la Kwanza kuvunja kambini baada ya ligi yao kumalizika, hivyo tumekuwa na changamoto ya kupata timu ya kucheza nayo"

"Tuna matumaini ndani ya wiki hii kupata timu ya ligi ambayo tutacheza nayo. Mechi hiyo itampa kocha mwanga wa kuona yale aliyokuwa akiyatoa kwenye mazoezi yamefanyiwa kazi, lakini pia kuwapa nafasi wachezaji ambao hawakupata nafasi katika mechi zilizopita za ligi," alisema Mfikirwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
47m ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
12h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
16h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
21h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’