Kikosi cha Yanga U20 kinahitaji alama moja tu katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mwadui Fc kutinga nusu fainali ya ligi kuu ya Vijana inayofanyika jijini Dar es salaam uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Jana Yanga iliondoka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania na kufikisha alama nne wakiwa kileleni mwa kundi A
Watani zao Simba nao walishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Mwadui Fc ambao tayari wameondoshwa katika michuano hiyo baada ya kupoteza mechi zao mbili za kwanza
Wakati Yanga ikimaliza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mwadui Fc, Simba wataikabili timu ngumu ya JKT Tanzania inayoshika nafasi ya tatu ikiwa imekusanya alama tatu
Β
ADVERTISE HERE