Kibu kupewa miaka minne Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jun 2021
Kibu kupewa miaka minne Yanga

Yanga ilianza kumfuatilia mshambuliaji wa Mbeya City Kibu Denis hata kabla hajaitwa kuitumikia timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'

Wengi walikubali uwezo wake baada ya mchezo wa timu ya Taifa dhidi ya Malawi uliomalizika kwa Tanzania kushinda mabao 2-0

Katika mchezo huo, Kibu ndiye aliyesababisha mabao yote mawili kupatikana, akitengeneza bao la kwanza na kufanyiwa madhambi yaliyopelekea bao la pili kupatikana

Imeelezwa Yanga imemalizana na Mbeya City juu ya usajili wa mshambuliaji huyo aliyefungia Mbeya CityΒ  mabao saba ligi kuu ya Vodacom msimu huu

Kibu anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria

Katibu Mkuu wa Mbeya City Emmanuel Kimbe amethibitisha Yanga kumuhitaji mshambuliaji huyo na kuwa wamekamilisha mazungumzo

Kimbe amedokeza kuwa Kibu atawagharimu Yanga takribani Tsh Milioni 180 kuweza kujiunga nao kwa mkataba wa miaka minne

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’