Hatujapokea barua ya Lamine - Bumbuli

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jun 2021
Hatujapokea barua ya Lamine - Bumbuli

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa bado hawajapokea barua ya beki Lamine Moro anayedaiwa kuomba kuondoka Yanga

Viongozi wa Yanga jana walikutana kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji kujadili masuala mbalimbali yanayoihusu klabu

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema mpaka wanamaliza kikao hicho, hawakuona barua ya Lamine

"Hizo habari tunaziona tu na kuzisoma kwenye mitandao lakini leo (jana) ndio siku ambayo kulikuwa na kikao cha kamati ya utendaji, tumekaa ofisini siku nzima hatujaiona hiyo barua, labda anatarajia kuileta lakini kwa sasa sisi hatujaipata barua ya Lamine kutaka kuondoka," alisema Bumbuli

Kumekuwa na maoni tofauti ya mashabiki wa Yanga huku wengi wakiutaka uongozi waachane na nahodha huyo kama ameomba mwenyewe

Kwa sasa Yanga haina changamoto katika eneo la ulinzi wa kati, Dickson Job, Bakari Nondo wakifanya vizuri wakati Abdallah Shaibu akiendelea kuuguza majeraha

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17m ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
18h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
19h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’