Mambo matano muhimu mchakato wa Mabadiliko Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jun 2021
Mambo matano muhimu mchakato wa Mabadiliko Yanga

Mambo muhimu matano (5) unayopaswa kuyafahamu kuhusu mabadiliko ya Yanga.

Aina ya Kampuni:

Kamati ya Mabadiliko inapendekeza kampuni binafsi ili iweze ku-control wamiliki wake kuwa wanachama na mashabiki wenye vinasaba na Yanga tu, Kwenye Kampuni ya Umma, kila mtu angeweza kununua hisa na kuwa sehemu ya umiliki ata kama sio mwana Yanga. Hii ni kuhakikisha Klabu ya Yanga inamilikiwa na wanayanga tu

Makubaliano Maalumu:

Yanga itatengeneza makubaliano maalumu (Standard Shareholders Agreement (MOU) ambayo yataainisha masharti maalumu ya uwekezaji na kuzingatia miiko na tamaduni za Yanga. Kila muwekezaji atabidi akubaliane na masharti hayo ndio atauziwa hisa.

Kwa upande mwingine, makubalinao haya yamelenga kulinda tamaduni na miiko ya Yanga ambayo kwa kitaalamu tunayaita (Grundnorms).

Tamaduni hizi zimekuwepo toka uanzishwaji wa Yanga. Kwa mfano, Muwekezaji hawezi kutubadilishia nembo, rangi, jina, au kuhamisha makao makuu n.k bila ridhaa ya Wanachama wa Yanga.

Hizi ni baadhi tamaduni zimeainishwa kwenye ibara ya 1, 2, 3 na 4 ya Katiba ya Yanga ya mwaka 2010.

Wajumbe wa kudumu wa bodi:

Klabu ya Yanga kupitia Mkutano Mkuu itachagua Baraza la Wadhamini, Wajumbe wa Excom, Rais wa Klabu na Katibu Mkuu kwa ajili ya kuendelea kusimamia Klabu ya Yanga nje ya majukumu ya kampuni itakayoanzishwa.

Kamati ya Mabadiliko inapendekeza Rais wa Klabu atakayechaguliwa, Katibu Mkuu na Mjumbe mmoja wa Baraza la wadhamini kuwa wajumbe wa Kudumu wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni itakayoanzishwa, pia wanachama watachagua wajumbe wengine wawili kwenye mkutano mkuu kwenda kuungana na wajumbe 3 wa kudumu kufika wajumbe 5 watakao ingia kwenye bodi ya wakurugenzi wa Kampuni

Mfumo wa Uwekezaji:

Hakuna mtu atakayekuwa muwekezaji kwenye Klabu ya Yanga bila kuweka pesa mezani kwa njia ya kununua hisa (share subscription) hisa atakazozinunua ndizo zitakazompa uhalali wa kuhesabika kama muwekezaji kwenye kampuni itakayofunguliwa na Yanga -

Umiliki wa hisa kwa Matawi ya Yanga:

Matawi ya Yanga yanatambulika kwa mujibu wa ibara ya 62 ya Katiba ya Yanga, hivyo basi Wanachama wa Yanga wanaweza kununua hisa kupitia matawi yao au mwanachama mmoja mmoja.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’