Mwenyekiti wa zamani klabu ya Yanga Yusufu Manji amesema anajisikia faraja kurejea nyumbani baada ya muda mrefu kupita
Manji amesema aliacha moyo wake Jangwani na amefurahi kupewa mwaliko wa kushiriki Mkutano Mkuu leo
"Nashukuru nimerudi nyumbani. Kiasi nilichoacha Jangwani ni moyo wangu. Kwa hiyo naheshimu maoni yenu, nashukuru kwa kualikwa hapa leo, Nawatakia kila la kheri na mbele ya safari nitajaribu kushiriki," alisema Manji baada ya kuombwa kuwapa neno Wanachama
Ujio wa Manji uliibua shangwe na nderemo kutoka kwa Wanachama ikiwa ni takribani miaka minne imepita tangu Manji aliposhiriki harakati za Yanga
ADVERTISE HERE