Hatutakuwa daraja lao - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jun 2021
Hatutakuwa daraja lao - Nabi

Baada ya kurejea jijini Dar es salaam kutoka Tabora ambako walifanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United, kikosi cha Yanga kilielekea moja kwa moja kambini Kigamboni kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba

Mchezo huo utaunguruma siku ya Jumamosi, Julai 03 kunako dimba la Benjamin Mkapa

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi, amesema kikosi chake kimahesabu bado kiko kwenye mbio za kuwania ubingwa

Amesema ligi bado haijamalizika na katika mpira lolote linaweza kutokea

Lakini muhimu zaidi hawatakuwa tayari kuwa daraja la watani zao Simba kutangaza ubingwa

"Ni mechi ngumu na ushindani mkubwa kwa sababu kila mmoja wetu tunahitaji matokeo, kwetu ni lazima tushinde mechi hii kwa sababu bado tuko katika mbio za ubingwa na hatutaki kuwa daraja la wapinzani wetu kutangaza ubingwa kupitia mchezo huo," alisema Nabi

Tangu alipotua mwezi April kuchukua nafasi ya Kocha Cedric Kaze, Nabi amefanikiwa kukiimarisha kikosi cha Yanga hasa katika eneo la ushambuliaji

Chini yake, Yanga imefungwa mchezo mmoja tu na kutoka sare mchezo mmoja

Mchezo pekee aliopoteza ni mchezo wake wa kwanza kabisa baada ya kuanza majukumu yake dhidi ya Azam Fc na sare aliyopata ni kule Ruangwa ambako Yanga ilikataliwa bao halali lililopelekea mwamuzi kufungiwa

Amewaongoza Wananchi katika michezo nane, ushindi michezo sita

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’