Timu kusajili wachezaji 40 michuano ya CAF

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jul 2021
Timu kusajili wachezaji 40 michuano ya CAF

Tangu msimu uliopita Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) liliruhusu klabu zinazoshiriki ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho kusajili hadi wachezaji 40 badala ya 30

Ni kutokana na changamoto ya janga la corona ambalo bado linatikisa dunia

Msimu huu pia CAF imeruhusu klabu kusajili wachezaji 40 kwa ajili ya michuano hiyo

Pamoja na kuwa nyota wa kigeni wanaoruhusiwa kushiriki ligi ya ndani ni 10, TFF imeziruhusu timu zitakazoshiriki michuano ya CAF kusajili wachezaji wa kigeni zaidi ya 10 lakini watakaoandikishwa kwa ajili ya kushiriki ligi kuu idadi haitabadilika (10)

Hivyo haitashangaza kama itatokea Yanga ikasajili zaidi ya wachezaji 10 wa kigeni kwani wengine wanaweza kutumika kwenye michuano ya CAF tu

Kulingana na kalenda iliyotolewa na CAF kwa ajili ya michuano ya msimu ujao, mechi za hatua ya awali zinatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi wa tisa

Hivyo ni wazi ligi itakapomalizika wiki ijayo wachezaji hawatakuwa na muda mrefu wa kupumzika, watapaswa kuingia kambini kujiandaa na michuano hiyo

Lakini pia, ikumbukwe mwanzoni mwa mwezi wa nane kuna tukio la wiki ya Mwananchi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’