Mshambuliaji wa Yanga Waziri Junior amesema wamejipanga kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc kuhakikisha wanashinda mchezo huo hapo
Junior amesema mara nyingi mchezo dhidi ya timu inayopigania kujinusuru kuteremka daraja unakuwa mgumu hivyo wanahitaji kujituma zaidi ili kuweza kupata matokeo
"Sisi kama wachezaji tumejiandaa vizuri kwa sababu unapocheza na timu ambayo ipo kwenye hatari ya kuteremka daraja mechi inakuwa ni ngumu," alisema Junior katika mkutano na wahabari kuelekea mchezo huo
Mshambuliaji huyo aliyetua Yanga kutoka klabu ya Mbao Fc, amesema msimu huu hakuweza kutimiza malengo aliyokuwa amejiwekea jambo ambalo hakulifurahia
"Ligi bado haijaisha tuna mechi mbili, nilikuwa na malengo ya kuwa mfungaji bora. Mpaka sasa anayeongoza amefunga mabao 15, na mimi msimu uliopita nilifunga mabao 13, ni kitu kinachoniuma kwani pengine ningeweza kutimiza malengo yangu," alisema Waziri
Msimu huu Waziri amefunga mabao mawili katika dakika 156 alizoitumikia Yanga
Pengine atapewa nafasi katika michezo miwili iliyobaki kukamilisha msimu